Mkuu wa mkoa wa Iringa aipokea AGAPE (WUEMA) kwa kishindo

Baba askofu mkuu wa kanisa na taasisi ya AGAPE (WUEMA) ambaye pia ni makam wa askofu mkuu Afrika mashariki adhuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Mafenza kwa mazungumzo mafupi kuhusu kupatikana kwa hati za maeneo yaliyotolewa na serikali   kwa  taasisai  na kanisa la Agape (WUEMA) kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya shule na hospitali






Pichani ni baadhi ya viongozi wa kanisa la Agape wuema mkoa wa Iringa wakiwa ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa iringa Mh Amina Mafenza

Baada ya ziara  ya Askofu  mkuu wa  Tanzania Martin W. Gwila kwa mkuu wa mkoa Iringa Mh Amina Mafenza,  Askofu Gwila aliweza kusimika viongozi wa  Agape (WUEMA) mkoa wa Iringa  waliosimikwa ni pamoja na Askofu mkuu wa mkoa huo Askofu Emanuel Daniel Kanemba ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya Agape mkoani hapo  tarehe 01/11/2016 .Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Askofu msaidizi wa mkoa,katibu wa mkoa ,katibu msaidizi wa mkoa,mweka hazina wa mkoa ,mweka hazina msaidizi wa mkoa,wajumbe wawili na wachungaji wa wilaya zote za mkoa huo 
Baba Askofu mkuu wa kanisa na taasisi ya AGAPE (WUEMA) ambaye pia ni makam wa Askofu mkuu waAfrika mashariki wakwanza upande wa kushoto akiwa na Askofu wa Agape (WUEMA)mkoa wa Iringa Askofu  Emanuel Daniel Kanemba aliye vaa suti nyeupe /wapili upande wa kushoto pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo  Tarehe 01-11-2016











Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment