Ziara ya Askofu mkuu wa Agape tanzania mkoani dodoma

MSAFARA WA  AGAPE WUEMA NYUMBANI KWA MWESHIMIWA SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI
Msafara ulikua na viongozi kitaifa na kimataifa kitaifa alikwepo mkuu wa msafara ambaye ni Askofu mkuu wa Taasisi  na Kanisa la Agape wuema Tanzania Askofu willison Martin Gwila akiwa pamoja na mke wake mama Joyce Gwila ambaye amefunga kitambaa cha rangi ya pinki kichwani ,Agape Administrator,katibu mkuu baadhi ya  maaskofu wakuu wa mikoa (Kagera Dodoma,Arusha)na baraza la wazee kama waziri mstaafu mzee kiula.lakini viongozi kutoka nje ya nchi alikuwepo katibu mkuu wa Afrika,na Askofu mkuu wa Afrika mashariki Askofu Kaduyu Frank wote kutoka nchi jirani ya Uganda.
Msafara huo ulifika hadi nyumbani kwa spika wa bunge job Ndugai mkoani Dodoma kwenda kutoa shukrani ya Dhati kwa mheshimiwa spika wa bunge kutokana na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuuendelea kuunga mkono shughuli za Taasisi na kanisa la Agape wuema Tanzania kama kutoa maeneo ya kujengea miradi ya  makanisa nyumba za wachungaji ,viwanda,mashule pamoja na hospitali za rufaaa nchini kote

upande wa kulia ni mheshimiwa spika Job Ndugai na mke wake akifuatiwa na  AgapeAdministrator na upande wa kushoto ni Askofu mkuu wa Taasisi na kanisa la Agape Tanzania Askofu Willison Martin Gwila pamoja na mke wake wakiwa kwenye mazungumzo nyumbani kwa Spika wa Bunge la Tanzania mkoani Dodoma
Askofu mkuu alisema kuna zaidi ya hekari Elfu kumi na mbili (12000) hadi sasa ambozo serikali ya tanzania imeweza kutoa kwa mikoa mbalimbali kwaajili ya miradi ya Taasisi hiyo hapa nchini,Askofu willison alisema kuna haja kubwa ya serikali kuwaizinishia hati za baadhi viwanja ili kurahisisha na kuharakisha ujenzi wa huduma zinazolengwa kutekelezwa na taasisi ya Agape .





Askofu mkuu willison Martini Gwila alimkabidhi mheshimiwa wa bunge la Tanzania  Gob Lugai zawadi ya cheti

Pamoja na hayo Askofu mkuu willison Martini Gwila alimkabidhi mheshimiwa wa bunge la Tanzania George Lugai zawadi ya cheti cha  Tanzania kupewa nafasi ya kwanza(1)Afrika na nafasi ya 68 Duniani kutoka makao makuu ya taasisi hiyo nchini marekani  kwa kupewa huduma na mkuu wa taasisi ya World United Evangelical Ministries Aliance( wuema  )

Mheshimiwa Job Ndugai akionesha Cheti




Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment